by United Nations
Email Addresses
1 available
Phone Numbers
0 available
April 16, 2025
Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limesema kwa kuzingatia sera yake jumuishi, nchi hiyo inakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi Shirika hilo la wakimbizi limesema katika makazi kama Mayukwayukwa na Maheba ambayo ni moja ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Zambia familia za wakimbizi zilizolazimika kukimbia makwao zinajumuishwa ili ziweze kujikimu na kuishi kwa utangamano na wenyeji wanaowahifadhi. Moulid Hujale, ni afisa habari msaidizi wa UNHCR anasema “Selikali ya Zambia inajumuisha wakimbizi katika huduma za kitaifa kama vile elimu na hata programu za msaada wa kilimo ili kuongeza uzalishaji” Amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo Zambia imeonesha mshikamano wa dhati kwa jamii hizo za wakimbizi kwa kuhakikisha kuwa wanapata fursa ya kujenga upya maisha yao, kujikwamua kiuchumi na kuishi kwa heshima.Hata hivyo, UNHCR inasema nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika pamoja na ukarimu wake bado inakumbwa na athari za ukame mkali uliotishia uhakika wa chakula na kuyumbisha uchumi na katika hatua za kukabiliana na hali hiyo, Moulid ansema “UNHCR inashirikiana na serikali ya Zambia kuunganisha makazi ya wakimbizi kwenye gridi ya taifa ya umeme. Tunajua muundo huu wa ujumuishwaji na maisha endelevu vinagharimu fedha, Lakini hiki ndicho hasa wakimbizi wanachokihitaji, hivyo tunahitaji msaada wako ili kufanikisha hili”. Licha ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Zambia katika kuwakirimu wakimbizi, UNHCR imeonya kuwa uhaba wa fedha inaokabiliwa nao unatishia kuathiri mafanikio hayo na hasa utoaji wa huduma muhimu kwa familia hizo zilizolazimika kufungasha virago na kusaka usalama Zambia. Sasa limetoa ombi la msaada wa haraka wa kimataifa ili kuendelea kufanikisha huduma za kuokoa maisha zinazohitajika sana na wakimbizi hao.
April 16, 2025

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika masuala ya afya hususan harakati za kukabiliana na majanga yajayo ya afya; wakimbizi huko Zambia ambako sera jumuishi zimewajengea uwezo; Jukwaa la vijana na mchango wa sanaa kwenye usawa na utengamano.

Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo huko mjini Geneva, Uswisi, nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi ujao wa Mei. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi.

Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, likiongeza kwamba kwa kuzingatia sera jumuishi ya Zambia, taifa hilo linakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi.

Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) limeanza jana hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na litamalizika kesho tarehe 17 Aprili. Vijana kutoka nchi mbalimbali wamehudhuria jukwaa hilo akiwemo Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amehojiwa na Leah Mushi wa Idhaa hii. Kapwani anaanza kwa kueleza umuhimu wa mikutano hii.

Gislain Kalwira, Muandaaji wa tamasha la Musika na Kipaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linalofanyika kila mwaka kuleta pamoja wasanii wa kike na wa kiume wa fani mbalimbali, kwa kutambua kuwa jana dunia imeadhimisha siku ya sanaa duniani. Kalwira kupitia video iliyochapishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, anafafanua mantiki ya tamasha hilo na kujenga usawa kijinsia.

April 16, 2025
Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo Geneva, Uswisi, Nchi Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi Mei mwaka huu wa 2025. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi. "Leo mataifa ya dunia yameandika historia mjini Geneva," amesema Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO na kuongeza kwamba, "kwa kufikia makubaliano kuhusu Mkataba wa Majanga ya kiafya, siyo tu wameweka msingi wa makubaliano ya kizazi hiki yanayolenga kuifanya dunia kuwa salama zaidi, bali pia wameonesha kuwa ushirikiano wa kimataifa bado uko hai, na kwamba hata katika dunia iliyogawanyika, mataifa bado yanaweza kushirikiana kutafuta mwafaka na mwitikio wa pamoja dhidi ya vitisho vya pamoja.” Mwezi Desemba mwaka 2021, wakati janga la COVID-19 likiwa limepamba moto, Nchi Wanachama wa WHO ziliunda Mamlaka ya Majadiliano ya Kiserikali ili kuandaa na kujadiliana kuhusu mkataba, makubaliano au nyenzo nyingine ya kimataifa, chini ya Katiba ya WHO, kwa ajili ya kuimarisha uzuiaji, maandalizi na hatua dhidi ya majanga ya kiafya. Mapendekezo katika rasimu iliyotayarishwa ni pamoja na: kuchukua hatua madhubuti za kuzuia majanga ya kiafya kwa kutumia mbinu ya Afya Moja; kujenga uwezo wa utafiti na maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani; kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na maarifa, ujuzi na utaalamu unaohusiana na uzalishaji wa bidhaa za afya zinazohusiana na majanga ya kiafya; kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha maandalizi, utayari na uimara wa mifumo ya afya; na kuanzisha mtandao wa kimataifa wa mnyororo wa usambazaji na vifaa. Pendekezo hilo linathibitisha mamlaka ya nchi kushughulikia masuala ya afya ya umma ndani ya mipaka yao bila kuingiliwa.
Pod Engine is not affiliated with, endorsed by, or officially connected with any of the podcasts displayed on this platform. We operate independently as a podcast discovery and analytics service.
All podcast artwork, thumbnails, and content displayed on this page are the property of their respective owners and are protected by applicable copyright laws. This includes, but is not limited to, podcast cover art, episode artwork, show descriptions, episode titles, transcripts, audio snippets, and any other content originating from the podcast creators or their licensors.
We display this content under fair use principles and/or implied license for the purpose of podcast discovery, information, and commentary. We make no claim of ownership over any podcast content, artwork, or related materials shown on this platform. All trademarks, service marks, and trade names are the property of their respective owners.
While we strive to ensure all content usage is properly authorized, if you are a rights holder and believe your content is being used inappropriately or without proper authorization, please contact us immediately at [email protected] for prompt review and appropriate action, which may include content removal or proper attribution.
By accessing and using this platform, you acknowledge and agree to respect all applicable copyright laws and intellectual property rights of content owners. Any unauthorized reproduction, distribution, or commercial use of the content displayed on this platform is strictly prohibited.